Kumbe hii ndiyo sababu iliyomfanya Jorginho kutua Chelsea na kuachana na Man city - Darajani 1905

Kumbe hii ndiyo sababu iliyomfanya Jorginho kutua Chelsea na kuachana na Man city

Share This

Chelsea ilifanikiwa kumnasa Jorginho Frello kutoka klabu ya Napoli ya nchini Italia karibu miezi miwili iliyopita. Akitua Chelsea muda mfupi toka aliyekuwa kocha wake klabuni Napoli alipotangazwa rasmi kwamba ni kocha mpya wa Chelsea akirithi mikoba ya kocha muitaliano mwenzake, Antonio Conte.

Lakini kutua kwake Chelsea kulionyesha kuzua zogo kubwa haswa kutokana na nyota huyo kukaribia kujiunga na klabu ya Manchester city ambayo kocha wake Pep Guardiola alikiri na kusema kwamba alikuwa akimuhitaji mchezaji huyo lakini janjajanja ya Chelsea ikabadilisha mambo.

Je nini kilitokea kilichomfanya muitaliano huyo mwenye uraia wa Brazil kukubali kujiunga na Chelsea na kuachana na klabu ya Manchester city? swali hilo alilijibu wakala wa nyota huyo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na moja ya vyombo vya habari nchini Italia.

"Alikuwa ameshafikia makubaliano binafsi na klabu ya Man city, lakini klabu hiyo ilishindwa kufikia makubaliano na klabu ya Napoli hali iliyosababisha Chelsea kutumia upenyo huo kumnasa"

"Anaendelea vizuri na ana maisha mazuri pale Chelsea. Wamefanikiwa kushinda michezo yote minne. Lakini kujua kwake vizuri kuzungumza kiingereza kumemfanya kuwa na maisha marahisi na kupazoea kwa haraka" alisema wakala huyo.

Jorginho amekuwa muhimili mkubwa katika klabu ya Chelsea akitumika kama mtu wa kati anayechezesha timu na kuanzisha mashambulizi.

No comments:

Post a Comment