Ripoti kamili ya michezo ya kitaifa, nini kimejiri kwa wachezaji wa Chelsea - Darajani 1905

Ripoti kamili ya michezo ya kitaifa, nini kimejiri kwa wachezaji wa Chelsea

Share This

Usiku wa jana kulianza rasmi michuano mipya ya barani Ulaya ambapo timu za taifa la bara hilo zimeanzishiwa ligi yao ambayo imebatizwa jina la Ligi ya Kitaifa ya UEFA yaani UEFA Nations League ambayo hii ni mara ya kwanza kufanyika.

Michuano hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuzivutia televisheni ambazo zilikuwa haziwekezi kwenye michezo ya kirafiki ya timu za taifa wakidai hazina masoko sana na pia ili kuwavutia mashabiki ambao walikuwa wakidai kwamba michezo ya kirafiki haina mvuto.

Michuano hii itaenda kwa mfumo wa makundi mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu uku timu shiriki yakiwa yale mataifa yaliyo chini ya chama cha soka barani Ulaya maarufu kama UEFA ambazo zipo nchini 55.

Sasa jana kulichezwa michezo kadhaa lakini hapa nakuletea michezo ile iliyowahusisha nyota wa klabu ya Chelsea.

Wales 4-1 Ireland
Nyota wa Chelsea, Ethan Ampadu alifanikiwa kuiongoza timu yake ya taifa ya Wales hapo jana wakiibamiza timu ya Ireland jumla ya magoli 4-1 uku Ampadu akitengeneza goli moja kwa kutoa pasi ya mwisho. Nyota huyo aliichezea mchezo wa kwanza timu yake hiyo iliyochini ya kocha Ryan Giggs.

Ujerumani 0-0 Ufaransa
Mchezo huu ulikuwa ukiwahusisha nyota watatu kutoka klabuni Chelsea. Antonio Rudiger kwa upande wa Ujerumani na Olivier Giroud pamoja na N'Golo Kante kwa upande wa Ufaransa. Mchezo uliisha kwa sare tasa isiyokuwa ya magoli lakini N'Golo Kante akionekana kucheza kwa mtindo tofauti na uliozoeleka akitumika kukaba sana lakini sasa anaonekana kuyazoea maisha ya klabuni Chelsea akiwa chini ya kocha Sarri ambaye amembadilisha majukumu ya kukaba sana na kumpa majukumu ya kushambulia. Na hivyo ndivyo alivyoonekana kwenye mchezo wa jana akionekana akitimiza sana majukumu ya kukaba tofauti na mwanzo.

Jamhuri ya Czech 1-2 Ukraine
Tomas Kalas, nyota wa Chelsea anayecheza kwa mkopo kwenye klabu ya Bristol city kutoka nchini Uingereza jana alikuwa uwanjani kuiongoza timu yake ya taifa ya Jamhuri ya Czech kwenye mchezo huo wa kimataifa ingawa uliisha kwa kupoteza.

Michezo ya leo:
Usiku wa leo kunachezwa tena michezo ya kitaifa inayowahusisha nyota wa Chelsea ambapo Jorginho Frello, Emerson Palmieri na Davide Zappacosta wanaweza kupata nafasi kwenye timu ya taifa ya Italia hii leo kucheza dhidi ya Poland. Mchezo utakaochezwa saa 21:45 kwa saa za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment