Ni mfululizo wa fununu unaendelea mpaka sasa juu ya kipi kitaenda kutokea kuhusu nyota wazamani wa klabu ya Chelsea, John Terry ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu kadhaa licha ya usajili wa dirisha kubwa barani Ulaya kufungwa.
Mwanzoni kulitoka taarifa kwamba kocha wa klabu ya Aston Villa, Steve Bruce kuuambia uongozi wa klabu hiyo kwamba anamhitaji kwa mara nyengine tena gwiji huyo ambaye msimu uliopita aliitumikia klabu hiyo kwa msimu mzima kabla ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja.
Lakini wakati hilo likizidi kuendelea, ikatolewa taarifa kwa mara nyengine tena kwamba nyota huyo anaweza kujiunga na klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno, lakini tu kama klabu hiyo itamilikiwa na tajiri Pedro Rodriguez (sio mchezaji wa Chelsea) lakini bado imeendelea kuwa tetesi.
Ila sasa, hii leo kumetoka taarifa mpya inayodai kwamba gwiji huyo mwenye miaka 37 anafanyiwa vipimo na klabu ya Spartak Moscow ya nchini Urusi.
Nyota huyo kwasasa hana klabu anayoichezea hivyo anaruhusiwa kujiunga na klabu yoyote kutokana na kutokuwa na mkataba unaomfunga.
No comments:
Post a Comment