Nyota wa klabu ya Chelsea ambaye ni raia wa nchini Hispania, Cesc Fabregas anaweza kuondoka klabuni hapo katika dirisha la mwezi Januari.
Taarifa zilizopo zinadai klabu ya nchini Italia, AC Milan wanamfukuzia nyota huyo ambaye hajaichezea Chelsea mchezo wowote wa ligi kuu Uingereza kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal.
Chelsea italazimika kumuuza nyota huyo aliyejiunga na Chelsea mwaka 2014 kutokana na nyota huyo kuwa katika mwaka wake wa mwisho katika mkataba wake klabuni hapo.
Fabregas anamaliza mkataba na Chelsea katika dirisha la usajili la kipindi cha kiangazi na kama Chelsea isipompatia mkataba mpya basi anaweza akaondoka bure.
Inasadikika kwamba Chelsea itakuwa tayari kumuuza nyota huyo mwezi Januari kabla ya kumaliza mkataba wake na kuondoka bure.
No comments:
Post a Comment