Kumekuwa na tetesi nyingi zikimhusisha aliyekuwa nahodha na nyota wa Chelsea, John Terry ambaye anahusishwa kujiunga na klabu kadhaa ambazo ni pamoja na Aston Villa ya nchini Uingereza, Celtic ya nchini Scotland, Sporting Lisbon kutoka nchini Ureno lakini sasa akihusishwa kwa karibu na klabu ya Spartak Moscow kutoka huko nchini Urusi ambako mwaka huu kumefanyika michuano mikubwa nchini humo, michuano ya Kombe la Dunia.
Taarifa za mwisho zinadai kwamba John Terry ameshafanyiwa vipimo tayari na anakaribia kusaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka wa pili uku mshahara wake ukipangiwa kufika paundi milioni 1.8 kwa mwaka.
Lakini je unajua sababu ya klabu hiyo kupewa nafasi ya kumnasa gwiji huyo mwenye miaka 37 kwasasa? basi unaambiwa sababu kubwa ni Antonio Conte.
Ndiyo ni huyuhuyu Antonio Conte ambaye alikuwa kocha wa Chelsea na kuiongoza kushinda mataji mawili katika misimu yake miwili aliyodumu akiwa kama kocha wa Chelsea.
Ipo hivi, kocha wasasa wa klabu ya Spartak Moscow, Massimo Carrera alishawai kuwa kocha msaidizi wa Antonio Conte pindi kocha huyo alipokuwa akiifundisha klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Italia.
Hivyo inaelezwa kwamba Conte ndiye aliyehusika kama mtu wa kati katika usajili huu wa gwiji huyu ambaye katika kipindi cha Conte klabuni Chelsea alianza katika michezo tisa tu.
No comments:
Post a Comment