Usiku wa jana kuamkia leo, nyota kinda wa Chelsea, Tammy Abraham ameweka rekodi mpya kwa kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka na mchezaji bora chipukizi kwenye tuzo za London Football ambazo hutolewa kwa timu za soka zinazopatikana jijini London.
Nyota huyo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwenye ligi kuu Uingereza akiwashinda wachezaji Gary Cahill (Crystal Palace), Heung-Min Son (Tottenham), Jorginho (Chelsea) na Pierre-Emerick Aubameyang (Arsenal).
Lakini pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi ambapo amechukua tuzo hiyo akiwashinda Bryan Mbeumo (Brentford), Fikayo Tomori (Chelsea), Gabriel Martinelli (Arsenal) na Mason Mount (Chelsea).
Mji wa London ndiyo mji mkuu nchini Uingereza na ndilo jiji lenye klabu nyingi za soka kuliko mji wowote nchini Uingereza ikikadiliwa kuwa na klabu za soka zaidi ya 40 jijini humo.
No comments:
Post a Comment