Katika maisha ujirani upo, nilianza kuwashukuru wenye nyumba ambao ni Mashabiki wa Chelsea, sasa ni zamu ya majirani wa mashabiki wa Chelsea.
Mafanikio ya blog ya Darajani 1905 ya kutimiza wanafamilia zaidi ya elfu kumi (10,000) toka kuanzishwa wiki moja juma haimaanishi ni mashabiki au wapenzi wa Chelsea peke yake ndio waliohusika katika hili, hapana kuna wapenda soka ambao wanahitaji kujua habari za klabu yoyote ingawa wao sio wapenzi na mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakiutumia ukurasa huu katika kuzipata habari hizo, nanyi nasema asante kwenu.
Kama we ni mmoja wa familia hii kubwa ya Darajani 1905 basi nakushukuru na naomba tushirikiane maana ili pawepo na amani kwenye mtaa basi ni muhimu kuwa na amani na majirani zako.
Najua kuna kutokupendezwa na vile navyoziita baadhi ya timu kama Man utd navyoiita Manyumbu, au Arsenal navyoiita Arsenyani, Liverpool navyoiita Liverpunga na ata Man city navyowaita Mama site, hakuna haja ya kukasirika wanafamilia. Ili ujirani uzidi kunoga na kuwa na utamu huwa kuna utani kama huu.
Asanteni Majirani zetu.
No comments:
Post a Comment