RUDIGER; NAIPENDA ROMA - Darajani 1905

RUDIGER; NAIPENDA ROMA

Share This

Mlinzi wa Chelsea, Antoinne Rudiger amejibu yale maswali yaliyokuwa yakisikika kuhojiwa juu ya mchezaji huyo kwamba kuondoka kwake Roma, Italia ambako alikuwa anaichezea klabu ya As Roma jijini humo ni kutokana na ubaguzi aliokuwa anafanyiwa.

Rudiger alisema "Sijaondoka Roma kwa vile nakimbia ubaguzi wa kule, ila nilifika Uingereza kwa vile nilikuwa na ndoto za kucheza hapa, napapenda Roma na nawaheshimu watu wa pale"

Rudiger amekuwa akikutana na ubaguzi wa rangi jijini Roma ambapo alitumia kucheza soka lake la kulipwa akiwa ndiye mlinzi aliyeongoza kutoa pasi ndefu msimu uliopita ambao kujiunga kwake na Chelsea amefika katika dirisha kubwa lililopita.

Ubaguzi wa rangi kwa wachezaji weusi unaelezwa kuwepo baadhi ya sehemu huku pia baada ya mchezo wa As Roma dhidi ya Chelsea katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya, klabu ya As Roma ilipewa adhabu kwa mashabiki wake kumuita Rudiger ni sokwe wakati akiwa ametokea timu yao.

No comments:

Post a Comment