CHELSEA INAMHITAJI LAMPARD MWENGINE - Darajani 1905

CHELSEA INAMHITAJI LAMPARD MWENGINE

Share This

Gwiji wa soka, Frank Lampard ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote klabuni Chelsea akiwa na magoli 211, japo alikuwa anacheza nafasi ya kiungo hivo ndivyo anavyotamani mkongwe mwenzake wa Chelsea, Denis Wise ambaye amesema ili Chelsea iwe sawa basi inatakiwa impate kiungo anayefunga magoli.

Denis Wise ambaye alikuwa nahodha wa Chelsea amesema "ili Chelsea iwe vizuri na iogopeke zaidi ya ilivyo sasa inatakiwa ipate kiungo mwenye kariba na ufundi wa kufunga kama ilivyokuwa kwa watu kama Frank Lampard, Michael Ballack na Michael Essien"

"Bakayoko na Kante ni kama wanacheza mpira unaofanana, Kante anatimiza majukumu yake kama inavyotakiwa, hivyo ni kama Bakayoko lakini Chelsea inamhitaji zaidi kiungo mwenye maamuzi na uwezo wa kufunga kama walivyofanya akina Lampard"

Chelsea itashuka uwanjani jumamosi hii kumenyana na Stoke city katika mchezo wa ligi kuu Uingereza ambapo ushindi unahitajika ili kujiweka sawa.

No comments:

Post a Comment