HERI YA KUZALIWA MJUKUU WA MENDOZA - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA MJUKUU WA MENDOZA

Share This

Tarehe 28-desemba mwaka 1990, katika jiji la Madrid huko nchini Hispania alizaliwa kijana mmoja aliyeitwa Marcos Alonso Mendoza au napenda kumuitaga mjukuu wa Mendoza.

Mjukuu huyo wa Mendoza alifika kwa mara kwanza Uingereza akiwa kama mchezaji wa Bolton Wanderers na baadae kurudi tena akiwa na Sunderland akiwa kama mchezaji wa mkopo, lakini sasa karudi tena Uingereza akitokea Fiorentina ya Italia na sasa yupo na Chelsea.

Jambo ambalo ulikuwa hulijui, katika miaka yote aliyoitumikia Fiorentina ambapo ndipo alikaa sana akiichezea michezo 85 akicheza toka mwaka 2013 mpaka 2016 na kufunga magoli 5 tu huku toka awasili Chelsea mwezi Agosti mwaka 2016 na huu ni mwaka 2017 tunaelekea 2018, hakuna beki au mlinzi aliyemzidi katika ufungaji ligi kuu Uingereza, mpaka sasa ameshafunga magoli 11.

Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa ya nyota huyo akiwa anatimiza miaka 27, hongera sana Mendoza.

No comments:

Post a Comment