Klabu ya Mama site (Man city) usiku wa kuamkia leo imeibamiza tena klabu ya Newcastle katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa goli 1-0, goli linaloifanya klabu hiyo kuizidi Chelsea inayoshika nafasi ya tatu kwa alama 16 huku klabu ya Manyumbu (Man utd) inayoshika nafasi ya pili ikiachwa alama 15.
Kutokana na ushindi wa Mama site unaifanya klabu hiyo iliyo chini ya Pep Guardiola kucheza michezo 18 bila kufungwa, ila ikicheza michezo 20 na kutoa suluhu mchezo mmoja na mengine akishinda yote. Lakini pia kwa ushindi huo unaifikia rekodi ya Chelsea ambapo mwaka 2008/2009, iliweka rekodi ya kutopoteza mfululizo katika michezo 11 ambapo Mama site ameivunja rekodi hiyo usiku wa leo lakini akisubiri kucheza dhidi ya Crystal Palace, na endapo ikishinda itakuwa imeweka rekodi mpya ya kucheza michezo 12 ugenini bila kufungwa.
No comments:
Post a Comment