Kuna habari zinadai kuwa Chelsea ina mpango wa kuachana na mlinzi wake David Luiz wakati ikwa na mipango ya kumleta mlinzi kutoka klabu ya Burnley.
Burnley ilimuuza mlinzi wake, Michael Keane aliyetimkia Everton na sasa imemfanya James Tarkowski kuwa kama mlinzi wao mahiri na ambaye amesaidia mafanikio makubwa ya Burnley msimu huu ikishuhudiwa wakiingia kwa mara ya kwanza kwenye klabu nne za juu katika ligi kuu Uingereza.
Sasa Chelsea imeifata klabu hiyo na kuonyesha nia ya kumsajili mlinzi huyo aliyezaliwa katika jiji la Manchester akitazamiwa kuwa mbadala wa David Luiz.
Tarkowski ambaye ni raia wa Uingereza mwenye asili ya kipoland kutoka kwa babu yake mpaka sasa ameshaichezea Burnley michezo 41 akijiunga nayo mwaka 2016.

CHESEA YAMFUKUZIA NYOTA WA BURNLEY
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment