Aliyewai kocha wa Chelsea ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Celtic ya nchini Scotland, Brendan ameihusia Chelsea juu ya mpangoo wake wa kutaka kumsajili nyota wa klabu yake ya Celtic, Moussa Dembele.
Chelsea imekuwa ikimfukuzia Dembele kwa karibu na sasa kocha huyo aliyewai pia kuzifundisha klabu za Swansea na Liverpunga (Liverpool) alisema "Toka nimefika hapa(Celtic) nimekuwa nikisikia mengi kuhusu Dembele kutakiwa na klabu kadhaa, ila mpaka sasa sijaona klabu ikifanya mawasiliano yoyote ili kumsajili nyota huyo"
"Hakuna mawasiliano yoyote yaliyofanyika kati ya klabu fulani kufanya mawasiliano na Dembele mwenyewe, kwa hiyo bado ni mchezaji wa Celtic, ingawa siwezi kusema mwezi januari (dirisha dogo la usajili) kama ataendelea kubaki, na kama akiondoka basi hilo ndio soka la kisasa" alisema Brendan.
Kwa maneno haya inaonyesha milango imefunguliwa kwa klabu yoyote haswa Chelsea kupeleka maombi yake kwa nyota huyo ili imsajili.

BRENDAN; CHELSEA FANYENI HARAKA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment