Michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 imebakiza ni muda mfupi tu kabla ya kuanza ambapo itafanyika nchini Urusi ambapo inategemewa kuanza mwezi Juni mwaka kesho.
Lakini kuna hatihati ya nyota wa Chelsea, Kenneth Omeruo ambaye kwa sasa anacheza klabuni Kasimpasa huenda akaikosa michuano hiyo. Taarifa zinadai kuwa kocha wa Nigeria, Gernot Rohr amepewa nfasi ya kuwachagua nyota 23 kati ya nyota 33 ambao wapo kwenye orodha yake ili wao ndio wasafiri kuelekea Urusi mwakani lakini kwa mlinzi huyo jambo jema ni kwamba kwenye orodha hiyo ya wachezaji 33 naye, Omeruo yumo.
Lakini kocha huyo tayari ameshawachagua nyota 15 na kubaki nyota 8 ili watimize idadi ya wachezaji 23 ambapo kati ya hao nane waliobaki , kocha Rohr amesema atawapima kutokana na michezo yao ya vilabu watakayocheza huku Omeruo akiwa kama mlinzi wa kulia anatakiwa acheze vyema katika michezo yakea atakayoichezea Kasimpasa ili aweze kumshawishi kocha amuingize kwenye kikosi.
Je atafanikiwa kuingia katika orodha ya wachezaji 25? Muhimu ni kumuombea kinda huyu wa Chesea.
NYOTA CHELSEA KULIKOSA KOMBE LA DUNIA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment