CARRASCO MLANGONI KWA CHELSEA - Darajani 1905

CARRASCO MLANGONI KWA CHELSEA

Share This
Nyota wa klabu ya Ubelgiji, Yannick Carrasco ambaye amekuwa akitajwa kuwaniwa na Chelsea, sasa dili hilo huenda likatimia mara baada ya nyota huyo kuonyeshwa mlango wa kutokea klabuni kwake Atletico Madrid.

Ripoti zinadai kuwa Carrasco amekuwa kwenye mgogoro na timu yake kutokana na kutokuwa na mawasiliano mazuri baina yake na baadhi ya wachezaji wa klabuni hapo na sasa inaonekana hakuna jambo la kuendelea kati ya nyota huyo na klabu yake.

Kuna ripoti pia zinadai nyota huyo aliyekuwa anasakwa na Chelsea kabla ya dili hilo kutokukamilika sasa anatajwa kutafuta klabu ya kumsajili na hataki kuendelea kubaki tena Atletico.

Nadhani hu ndio wakati nzuri kwa Chelsea kumsajili nyota huyo kutokana na kutafuta kwake klabu ya kuichezea inamaanisha kama Chelsea ikimfata basi hakutokuwa na kipingamizi kutoka kwa nyota huyo aliyewai kuichezea klabu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment