Mchambuzi wa michezo, Martin Keown amehoji akili na tabia ya mlinzi mpya wa klabu ya Liverpunga (Liverpool), Virgil van Dijk ambaye usajili wake wa kujiunga na klabu hiyo umekamilika jana kwa kiasi cha paundi milioni 75.
"Sidhani kama ana akili sahihi, hakufanya jambo zuri pindi alipokuwa Southampton haucheza mwezi wote wa kwanza wa ligi kuu na hata baada ya hapo amekuwa hajitumi, sizani kama alifanya jambo sahihi. Alitakiwa kuonyesha heshima kwa klabu yake." alisema Keown.
Van Dijk aliwai kuigomea klabu yake ya Southampton mara baada ya klabu hiyo kuingia kwenye mgogoro na Liverpunga na kutaka kufikia kuishtaki klabu hiyo kwenye chama cha soka ikidaiwa Liver kufanya mazungumzo na mlinzi wao bila kupata ruhusa kutoka kwa klabu yake ya Southampton, na wakati wote huo Van Dijk ndiye alikuwa akilazimisha usajili wake akitaka ajiunge na Liver.
Huenda kutocheza kwake kwa hali na bidii klabuni Southampton ilikuwa ni kuonyesha kukerwa kwa uhamisho wake wakujiunga na Liver kushindikana huku sababu ya kushindikana kwa usajili huo ikiwa ni klabu yake mwenyewe. Ikumbukwe kuwa chelsea nayo iliwai kupeleka maombi kwa klabu yake ili kumsajili nyota huyu.
VAN DIJK HANA AKILI
Share This
Tags
# Majirani
Share This
About Darajani 1905
Majirani
Labels:
Majirani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment