COURTOIS NJIANI KUELEKEA MADRID - Darajani 1905

COURTOIS NJIANI KUELEKEA MADRID

Share This
Kumekuwa na sintofahamau inayoendelea klabuni Chelsea ambapo kuna taarifa zinadai kusimamishwa kwa mazungumzo kati ya Chelsea na kipa wa klabu hiyo, Thibaut Courtois ambapo taarifa zinadai mazungumzo ya kuongezewa mkataba kwa nyota huyo sasa zimesimamishwa huku kukiwa na fununu kwamba nyota huyo amesema atasaini mkataba mpaka mwisho wa msimu.

Lakini kuna taarifa zinadai nyota huyo anaweza akajiunga na Real Madrid ambayo inatajwa kumuwania kipa huyo raia wa Ubelgiji huku sababu inayochochea usajili huo ikitajwa kutokana na familia ya nyota huyo ipo nchini Hispania katika jiji la Madrid ambako huko alipata mtoto pindi akiwa kwa mkopo Atletico Madrid.


Kwa upande wa Chelsea kunaelezwa kuwa ipo tayari kumpa mkataba mpya mlinda mlango huyo ambao utamfanaya kuwa kipa anayelipwa zaidi duniani ambapo atavuta mshahara wa paund 200,000 kwa wiki.

Mipango ya Real Madrid kwa sasa ni kumuuza kipa wake Keylor Navas abapo klabu hiyo inaelezwa ipo tayari kupokea ofa ili kumuuza kipa huyo ambapo kwa maana hiyo inafungua milango kwa Courtois ili atue klabuni hapo.

*Yani kama Courtois atafanikiwa kuisoma habari hii basi ajue Chelsea inamuhitaji kuliko anavyozani, amwambie ata Roman Abramovich aihamishe familia yake itoke Madrid ili imfate London

No comments:

Post a Comment