DIEGO COSTA HUYU HAPA - Darajani 1905

DIEGO COSTA HUYU HAPA

Share This
Mshambuliaji wa Chelsea ambaye anatarajiwa kujiunga rasmi na klabu ya Atletico Madrid katika dirisha hili la usajili la mwezi wa kwanza, Diego Costa anatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza klabuni hapo tarehe 3 ya mwezi januari mara baada ya kujiunga baada ya kutocheza mchezo wowote wa kiushindani toka mwezi Juni mwaka huu.

Diego Costa ambaye mpaka sasa anatambulika kama mchezaji wa Chelsea ingawa alishaachana na timu hiyo mara baada ya kuingia kwenye mgogoro na kocha wa Chelsea, Antonio Conte na kipindi chote hiki ameamua kujiunga na Atletico Madrid ambako huko hajacheza mchezo wowote wa kiushindani kutokana na klabu hiyo kuwa na adhabu ya kutokufanya usajili mpaka mwezi januari ambao ndio Costa nae ataruhusiwa kucheza.

No comments:

Post a Comment