Kila mtu anafurahishwa na kiwango cha nyota ghali wa Chelsea, Alvaro Morata kuanzia uwanjani na hata anavyoishi maisha yake kama mchezaji na nyota wa Chelsea.
Leo katika mitandao nimeona nikuletee moja ya ujumbe wa mke wa nyota huyo Alice Campelo ambaye aliutuma siku ambayo Chelsea ilimenyana dhidi ya Everton na Morata hakuwepo kwenye mchezo huo kutokana na adhabu ya kufungiwa mchezo huo.
Kutokana na adhabu hiyo, Morata aliamua kuzunguka na mke wake mitaani ambapo aliamua kutoka nae ili kuzunguka katika maduka mbalimbali.
Kupitia mtandao wa Instagram, Alice Campelo aliandika "Asante kwa kuwa pamoja nami kwa kila jambo, na hata kunisaidia na kunishauri. Mara zote umekuwa unapenda kunifanya niwe na furaha na kujaribu kuiweka furaha yangu juu yako lakini pia asante kwa kunifanya niwe wa pekee kwenye kila jambo lako na hata kwa kila mtu. Asante pia kwa kubadilika na kuwa mwanaume wa kustaajabisha na kuwa mwanaume yule niliyetamani kuwa nae, na mme wa ndoto zangu na hata baba wa watoto niliyemtamani"
Morata anategemea kupata mtoto kutoka kwa mke wake huyo aliyefunga nae ndoa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment