Mlinzi wa Chelsea aliyetolewa kwa mkopo katika ligi ya Bundesliga, Baba Rahman huenda akarejea kikosini tayari kumpa changamoto Marcos Alonso katika nafasi ya 'left wing-back' yaani mlinzi na winga wa kushoto.
Baba Rahman hajacheza mchezo wowote wa kiushindani toka mwezi februari mwaka huu mara baada ya kupata majeraha na sasa kuna taarifa zinasema anaweza akajiunga na kikosi cha Chelsea muda wowote mara baada ya kuanza mazoezi toka mwezi oktoba akijiweka sawa.
Chelsea imekuwa ikimfukuzia Alex Sadro katika nafasi hiyo ya mlinzi wa pembeni ingawa dili hilo limekuwa likisuasua, kwa maana hiyo kwa ujioa wa Baba huenda ukamfanya Antonio Conte aghaili kumsajili Alex Sandro.
No comments:
Post a Comment