CAPELLO AMKOSOA CONTE KWA BONUCCI - Darajani 1905

CAPELLO AMKOSOA CONTE KWA BONUCCI

Share This

Kocha raia wa Italia ambaye kwa sasa anaifundisha timu ya Jiangsu Suning iliyoko bara la Asia ambaye aliwai kukiri kuitaka kuifundisha Chelsea kabla kufika kwa Conte klabuni hapo, Fabio Capello amekaririwa akimkosoa mlinzi anayetakiwa na klabu hiyo, Leonardo Bonucci.

Fabio Capello ambaye kabla ya kufika kwa kocha Antonio Conte aliwai kukaririwa akisema anatamani kuifundisha Chelsea amesema kuwa mlinzi Bonucci hayupo vizuri kwenye ukabaji.

"Unapomzungumzia Bonucci, ni kati ya mabeki bora Italia akiwa na mpira miguuni, lakini tatizo lake kwenye ukabaji" alisema Capello aliyewai pia kuiongoza timu ya taifa ya Uingereza kwenye kombe la dunia mwaka 2010.

Antonio Conte amekuwa akitajwa kumfukuzia mlinzi huyo tangu akiwa Juventus kabla ya nyota huyo kusajiliwa na  AC Milan ambako huko anadaiwa kutokuwa na furaha kutokana na mwenendo wa klabu yake. Conte na Bonucci walishawai kuwa pamoja klabuni Juventus na timu ya taifa ya Italia, huku Conte akiwa kama kocha.

No comments:

Post a Comment