CHRISTENSEN AMFATA LUIZ - Darajani 1905

CHRISTENSEN AMFATA LUIZ

Share This
Jana wakati Chelsea iliposhuka katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Brighton ambao Chelsea ilishinda 2-0, kulishangazwa kwa kutokuwepo mlinzi, kinda anayefanya vizuri kwa sasa, Andreas Christensen.

Kuna maswali mengi yaliulizwa, imekuwaje kwa Christensen wakati hakukuwa na taarifa zozote kuhusu majeruhi ya nyota huyo.

Sasa mara baada ya mchezo huo, kocha Antonio Conte wakati akiwa anafanya mkutano na waandishi wa habari aliulizwa kuhusu imekuwaje kwa Christensen, naye alijibu "kama timu inabidi uwe na kikosi kipana, ili uweze kufanya mabadilishano kwa mchezaji maana katika michuano yote hii tunayoshiriki, haitokuwa vyema kwa mchezaji kucheza kila mchezo, tumemkosa David Luiz ambaye ni majeruhi, na leo(jana baada ya mchezo) tumemkosa Andreas Christensen ambaye alipata ugonjwa ghafla na kumfanya kushindwa kujumuika nasi"

"na kutokana na pengo lake, tumelazimisha kumweka Gary Cahill acheze kama mlinzi wa kati akiwa kati ya Rudiger na Azpilicueta, hii ni mara ya kwanza kufanya hivyo, lakini ni vyema zaidi kuliko kubadilisha mfumo" alisema Antonio Conte.

Kwa majeruhi hayo au ugonjwa huo wa Christensen unaifanya Chelsea kuwakosa nyota watatu ambao wanajiuguza ambao ni David Luiz, Charly Musonda nayeye mwenyewe.

*huenda Andreas Christensen kavimbiwa na pilau la sikukuu nini? hahaaaa natania, ila tunamuombea apone haraka ili arudi mapema, mashabiki tunamhitaji akiwa ndie mlinzi pekee aliyefululiza kufikisha pasi kwa 100% katika michezo mitatu, ndiye mlinzi pekee kufanya hivyo msimu huu ukiwatoa wale walioingia kama wachezaji wa akiba.

No comments:

Post a Comment