MORATA HAMUOGOPI HARRY KANE - Darajani 1905

MORATA HAMUOGOPI HARRY KANE

Share This

Kabla ya kutua Chelsea, mshambuliaji Alvaro Morata aliwai kuhusishwa na klabu kadhaa kwamba zinamfukuzia huku Manyumbu (Man utd) ikitajwa kama klabu inayoongoza katika kumuwania nyota huyo raia wa Hispania.

Lakini mara baada ya kutua Chelsea, kocha wa klabu ya Tottenham alisema "niliwai kufanya mawasiliano na Alvaro (Morata) na nikamwambia nahitaji ajiunga na Tottenham, naye alinijibu unanitaka mimi wakati tayari una Harry Kane" kauli ambayo ilitafsiriwa kwamba kukataa kwa Morata ni kuwa alikuwa akiogopa kuwa mbadala wa Harry Kane, ambaye ni mshambuliaji mkubwa wa klabu ya Tottenham.

Alvaro Morata amezijibu tuhuma hizo akisema sio za kweli na kuwa kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino alisema uongo, alisema Morata akiwa anahojiwa na Skysports.

"Hiyo sio sawa na ukweli ulikuwa hivi, kocha Pochettino alinipigia simu kuwa nijiunge na Tottenham naye akasema atatuchezesha wawili, yaani mimi na Kane tucheze pamoja, lakini nilimjibu kuwa kwa kipindi kile isingewezekana kutokana na Real Madrid(aliyokuwa anaichezea) iligoma kuniruhusu kuondoka" alisisitiza Morata.

Harry Kane ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa magoli kwa sasa katika ligi kuu Uingereza akiwa na magoli 18 huku Alvaro akiwa na magoli 10.

No comments:

Post a Comment