CONTE; HAZARD AFANYE MAAMUZI MWENYEWE - Darajani 1905

CONTE; HAZARD AFANYE MAAMUZI MWENYEWE

Share This

Kumekuwa na tetesi nyingi zikitajwa katika kipindi iki cha kuelekea mwezi Januari ambapo kutakuwa na dirisha dogo la usajili kwa ligi nyingi barani Ulaya.

Kuelekea katika dirisha hilo, Chelsea imekuwa ikitajwa sana juu ya kuondokewa kwake na nyota wake kama Eden Hazard anayetajwa kutakiwa na Real Madrid.

Na kuna taarifa zimetoka jana zikimuelezea baba wa nyota huyo anayetambulika kwa jina la Thierry Hazard zikidai baba mzazi huyo amesema mwanae amegoma kusaini mkataba mpya Chelsea ili aangalie nafasi yake ya kujiunga na mabingwa wa Hispania, Real Madrid.

Kocha wa Chelsea ametolea ufafanuzi zaidi kuhusu taarifa hizo akisema "kama navyozungumza kila siku kuwa jambo kama hili huwa lina mazungumzo binafsi kati ya mchezaji, wakala wa mchezaji na klabu yenyewe lakini kwa maoni yangu nadhani kama mchezaji unacheza kwenye klabu unayoona inamipango na mwendelezo mzuri basi ni vizuri kusalia hapo"

"sijasikia alichokisema wala kuona alichokiongea baba (baba yake na Hazard) lakini hata hivyo nadhani ni mtu mzuri ila nachoona kikubwa maamuzi yapo kwa nyota mwenyewe"

"kama akizani klabu inamfaa anaweza kubaki, ukizingatia bado ana muda zaidi wa kuonyesha kipaji na uwezo wake, na tusisahau Hazard ni mdogo kuliko Messi na Ronaldo" alisema kocha Antonio Conte

No comments:

Post a Comment