Nyota huyo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2017 kutoka Afrika na chombo cha habari cha Goal.com ambapo kimemchagua kuwa mchezaji bora akiisadia timu yake ya taifa kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 huko nchini Ursi lakini pia akiisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza akiwashinda nyota Pierre Aubameyang, Naby Keita, Mohammed Salah pamoja na Sadio Mane.
Nimekuwekea mfululizo wa baadhi ya aliyoyafanya ambayo kwake anaufanya mwaka 2017 kuwa ni mwaka bora kwake.
Victor Moses ameshuhudia kwa mara ya kwanza akibeba kombe la ligi kuu akiwa klabuni Chelsea ambapo lilitimia hilo mwezi May mwaka 2017 huku yeye akiwa moja ya watu muhimu katika mafanikio hayo ya klabu ikiwa chini ya kocha Antonio Conte.
Lakini pia kwa mwaka 2017 umemshuhudia Victor Moses akitimiza mchezo wa 100 akiichezea Chelsea toka aliposajiliwa akitokea klabuni Wigan Athletic na licha ya kutokuaminika mwanzoni huku akipelekwa mara kadhaa kwenye klabu kadhaa kucheza kwa mkopo lakini waka 2017 au msimu wa 2016/2017 umekuwa wa muhimu kwake akiaminiwa na kocha Antonio Conte na kuwa muhimili mzuri katika upande wa kulia akiwa kama winga-beko wa kushoto katika mfumo wa mafanikio wa kocha Antonio Conte wa 3-4-3. Alitimiza mchezo wake wa 100 katika mchezo wa ligi kuu alipocheza dhidi ya Brighton na mchezo kuisha kwa Chelsea kushinda 2-0 katika siku ya tarehe 26-Desemba.
Hongera kwako Victor Moses.

No comments:
Post a Comment