Kocha Antonio Conte alisema "Wanatakiwa wapate nafasi katika nafasi za chini za timu za vijana kwanza ili waweze kupata uzoefu wa kushika nafasi kubwa kwenye klabu" ambapo kwa kauli hiyo imepingwa na gwiji Wilkins anayedhani magwiji hao tayari wana uzoefu toka klabu hiyo ilipokuwa chini ya kocha Andre Villas Boas.
"Hapana,tayari wana uzoefu maana walishirikiana vyema tangu kwa kocha Villas Boas"
"unapokuwa mchezaji nyota na bora basi inabidi uishi na kuweka mambo yako hapo kwenye ubora wako. Nilimtazama Roy Keane (aliyekuwa mchezaji wa Man utd) aliposhuka na kwenda kufundisha klabu za chini nikajua tayari hakuna jambo kubwa angeweza kufanya maana isingewezekana tena kuwaua wachezaji nyota nakuwaelewa. John Terry anafaa kuwa kocha wa klabu ya Championship na Ligi kuu na sio aanzie chini maana atashindwa kuwaelewa nyota wakubwa wanataka na kuwaza nini maana tayari ashaanza na wachezajiwa chini" alisema Wilkins.
John Terry kwa sasa ni mchezaji wa Aston Villa inayoshiriki ligi daraja la kwanza au Championship ingawa kwa muda huohuo anasomea ukocha wakati Frank Lampard kwa sasa ni mchambuzi wa soka.


No comments:
Post a Comment