Wote tunakubaliana kuwa katika timu kipengele ambacho huwa kinaifanya timu iwe imara basi ni kipindi cha usajili.
Michael Emenalo ameshaondoka klabuni Chelsea, ambaye mashabiki walikuwa wanaulalamikia uongozi wake haswa katika kufanya kwake usajili, lakini sasa kuna kiongozi mwengine amechaguliwa ili ashike nafasi ya mghana uyo akishirikiana na mwanamama, Marina Glanovskaia kwenye nyanja ya usajili pale klabuni Chelsea.
Lakini kuna jambo litabaki tukimlaumu kocha na hata mwisho kumfukuza tukimpa lawama kwamba timu inafanya vibaya kumbe Chelsea yenyewe ndio imemfanya afanye vibaya.
Kwanini uongozi wa Chelsea usimpatie majukumu yote Antonio Conte afanye usajili mwenyewe kwa wale ambao anaona wanafaa kwenye timu? na sio kocha kuiambia bodi namtaka mchezaji huyu na yule ila mwisho wa siku klabu inawasajili wachezaji tofauti na wale aliowataka.
Katika dirisha kubwa la usajili, kocha Antonio Conte kuna nyota ambao aliwataka ambao hakuna hata mmoja aliyesajiliwa, Virgil Van Dijk alimtaka Conte ila klabu ikafanya tofauti, aliwataka pia akina Oxlade Chamberlain na Romelu Lukaku na hata Ross Barkley lakini wote hao hakuna hata aliyeletwa. Utamlaumu kocha kuwa timu inafanya vibaya wakati aliyemtaka hakuna aliyeletwa?
Kuna umuhimu gani wa usajili kufanya mtu mwengine wakati anayeiongoza timu kupitia kwenye michuano mbalimbali na ye ndio anaujua ugumu wa michezo ni kocha na mwisho klabu ikifanya vibaya anatimuliwa kocha?
Nadhani katika hili inabidi lifanyike jambo yasije yakamkuta kama kocha wa zamani wa Liverpunga (Liverpool), Brendan Rodgers kwa kulaumiwa klabu kufanya vibaya wakati usajili wa timu hafanyi yeye.
No comments:
Post a Comment