Kuelekea mchezo wa ligi kuu Uingereza leo jioni mishale ya saa 12 jioni kutakuwa na mchezo mkali pale Stamford Bridge ambapo Chelsea itashuka kumenyana na vijana wa Stoke city inayomilika na tajiri mmliki wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Bet365.
Hii ndio habari fupi kuelekea kwenye mchezo huo.
Andreas Christensen atarudi kwenye mchezo huu akitoka kwenye kuugua na kufanya kumkosa mchezo mmoja uliopita dhidi ya Brighton ambapo Chelsea ilishinda 2-0.
Huku majeruhi wakibaki kuwa walewale ambao ni David Luiz anayetegemewa kurudi kwenye mchezo wa kombe la FA siku ya tarehe 3-Januari huku pia kwa Charly Musonda maendeleo yakitajwa kuwa yanaendelea vizuri na huenda akarejea uwanjani kabla ya muda uliotegemewa kabla.
Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa ni Kelvin Friend ambaye mpaka sasa ameshakuwa mwamuzi katika michezo 16 huku akitoa kadi za njano 36 huku pia akihusika katika mchezo wa Chelsea ilipomenyana na Newcastle na The Blues ikishinda 3-1.
No comments:
Post a Comment