MORATA AMLETA ISCO LONDON - Darajani 1905

MORATA AMLETA ISCO LONDON

Share This

Nyota wa Chelsea ambaye ni raia wa Hispania, Alvaro Morata ametembelewa na rafiki yake ambaye ni nyota wa Real Madrid, Isco.

Isco amesafiri kutoka jijini Madrid ambapo alikuwa anacheza klabu moja na Morata kabla ya nyota huyo kusajiliwa na Chelsea ambapo pindi wakiwa wote walikuwa ni marafiki.

Kuja kwa Isco katika jiji la London kumeleta tafsiri tofauti haswa kwenye kipindi hiki cha kuelekea ufunguzi wa dirisha dogo la usajili ikisadikika huenda kutua kwa Isco kunaweza kuhusishwa na kutaka kujiunga na Chelsea, anayochezea rafiki yake, Morata.

Je unadhani Isco atafaa kuwa Chelsea?

No comments:

Post a Comment