Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Stoke city katika ligi kuu Uingereza, kocha Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari ambao tayari nishakuletea alichokisema katika mkutano huo na kama unataka kukisoma zaidi basi bonyeza hapa #ChelseaStoke
Lakini kati ya mambo ambayo Conte ameyaongea kwenye mkutano huo, aliulizwa pia kuhusu nyota wa klabu yake yaani Thibaut Courtois na winga Eden Hazard ambao wamekuwa wakitajwa kuhusiana na kuondoka klabuni hapo.
Alipoulizwa kuhusu Thibaut Courtois
Conte alijibu "Ni kipa bora duniani na na nafurahi kuwa naye na natamani pia kwa mmoja kati ya makipa wa Chelsea akishirikiana vyema na makipa Caballero pamoja na Eduardo. Mkataba wake utakuwa unaisha mwishoni mwa msimu ujao na nitapenda kuendelea kubaki nao zaidi. Ujue nini hili jambo ni mazungumzo ya binafsi kati ya mchezaji mwenyewe, wakala wake pamoja na klabu. Naamini kama ukiniuliza kama atabaki, nitakujibu ndiyo atabaki kwa kuwa tunamzungumzia kipa bora"
"sijui sana kuhusu familia yake iliyoko Madrid, lakini nna uhakika kama upo kwenye klabu kubwana unaiamini lazima utamani kuendelea kubaki. Kuendelea kucheza hapa sioni kama kuna tatizo na familia" alisema kocha Antonio Conte.
Alipoulizwa kuhusu Hazard
Conte alijibu "Jibu langu mara zote huwa ni moja, ni mazungumzo na maamuzi ya binafsi kati ya mchezaji, wakala na klabu. Ninajivunia kuwa nae, ni mtu mzuri na bado ana muda wa kuonyesha ubora wake" alisema Conte
Je unaonaje nafasi ya nyota hao kusalia klabuni? Toa maoni yako
No comments:
Post a Comment