MORATA KUREJEA JUVE? - Darajani 1905

MORATA KUREJEA JUVE?

Share This
Kuna taarifa mpya zimesambazwa zikimuonyesha nyota wa Chelsea, Alvaro Morata akiwa jijini Turin ambako kunapatoikana klabu ya Juventus ambayo aliwai kuichezea kabla. Nyota huyo akiwa na mke wake kwenye picha hiyo aliyoituma katika mtandao wa Instagram akisema akiwauliza wale wanaomfatilia (followers) kwenye mtandao huo kwamba "Je wanapenda arejee Juventus?" huku piaa akionyesha rangi kuu za klabu hiyo ambazo ni nyeupe na nyeusi na kuweka vikatuni vyenye kuonyesha kama kupenda ambapo hiyo ilitafsiriwa kwamba ni kama kuonyesha kwake mapenzi kutamani kurejea klabuni hapo siku moja.

 Alvaro Morata alicheza klabuni Juventus ambako huko alipata mafanikio makubwa wakati akiwa chini ya kocha Antonio Conte ambapo alicheza klabuni hapo na kufanikiwa kushinda mataji kadhaa yakiwemo ya ligi kuu Italia maarufu kama Serie A.


No comments:

Post a Comment