NYOTA CHELSEA KUREJEA UINGEREZA - Darajani 1905

NYOTA CHELSEA KUREJEA UINGEREZA

Share This
Moja kati ya nyota wa Chelsea aliyeutumia muda wake klabuni hapo bila mafanikio makubwa akibeba mataji ya ligi kuu Uingereza na kombe la ligi lakini hakupata muda mwingi wa kuichezea Chelsea ni huyu raia wa Ufaransa, Loic Remy ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Las Palmas amaye alienda klabuni hapo bure, akisaini mkataba wa miaka miwili, huuenda nyota huyo akaoondoka tena klabuni huko na kurejea ligi kuu Uingereza.

Kuna taarifa zinasema nyota huyo amekuwa akipata tabu kisiwani ambako klabu hiyo inapatikana nchini Hispania ambapo habari zinadai huwa anachelewa mara kadhaa kufika mazoezini kutokana na mlolongo mbaya wa visiwa vya Kanari ambapo klabu hiyo ya Las Palmas inapatikana.

Sio Loic Remy tu aliyeshindwa kudumu klabuni hapo kutokkana na hali ya visiiwa hivyo ila hata Kevin Prince Boateng ilimlazimu asitishe mkataba wake na klabu hiyo kutokana na hali ya visiwa hivyo.

Mchezaji huyo anahusishwa kutakiwa na klabu kadhaa kutoka Serie A lakini mwenyewe akipendelea kurudi Uingereza.

No comments:

Post a Comment