Ni siku nyengine tamu kwa mashabiki wa Chelsea mara baada ya kuishuhudia timu yao ikipata ushindi mnono dhidi ya Stoke city kwa magoli 5-0.
Alianza Antonio Rudiger aliyefunga kwa kichwa akipokea krosi ya Willian na kufunga goli hilo dakika ya 3'.
Goli la pili likifungwa na mwingereza, Danny Drinkwater aliyefunga kwa kupigaa shuti kali ambalo ndio goli lake la kwanza kuifungia Chelsea toka asajiliwe katika dirisha dogo.
Goli la tatu lilifungwa na Pedro aliyemchambua mlinzi wa Stoke city na kupiga shuti kali lililomfanya kipa Butland kuuangalia tu mpira bila kuufata na kuifanya Chelsea kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili kilianza huku Chelsea ikimiliki mpira kama kawaida na Chelsea kupata goli la nne kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Willian.
Goli la tano na la mwisho lilifungwa na Zappacosta aliyeingia kuchukua nafasi ya Victor Moses ambapo alifunga goli hilo dakika ya 88.
Jambo kubwa ambalo nimeliona leo ni kocha Antonio Conte kujaribu kubadilisha kikosi chake ili kuwaafanya wachezaji kupumzika ambapo kwa leo amempumzisha Eden Hazard ambaye hajacheza kabisa huku Bakayoko akiingia kuchukua nafasi ya N'Golo Kante. Nadhani ni njia nzuri kuweza kuifanya timu ipumzike ili ata pia iwe sawa kumenyana na Arsenal siku ya jumatano tarehe 3-Januari.
No comments:
Post a Comment