Chelsea inapoteza mchezo wake wa kwanza kwa mwaka 2018 huku ikikosa nafasi ya kucheza fainali ya kombe la Carabao, lakini pia, bado kocha Arsene Wenger anaendelea kutamba mbele ya kikosi cha Chelsea kilichochini ya kocha Antonio Conte ambapo katika michezo 8, Chelsea imepata ushindi mara moja ukiondoa ule mchezo wa kirafiki.
Lakini Chelsea ilikuwa ikicheza soka safi na kushindwa kutumia vyema nafasi ilizozipata huku Pedro akifunga goli ambalo lilikataliwa kutokana na kuonekana alizidi kabla ya baadae Eden Hazard kufunga goli safi, goli ambalo lilidumu kwa dakika kadhaa kabla ya kuchomolewa kwa Antonio Rudiger kujifunga kwa kichwa na kufanya mapumziko mchezo huo kuwa sare ya 1-1. Lakini Ross Barkley akicheza mchezo wake wa kwanza maalumu, akiingia kuchukua nafasi ya Willian aliyetoka kwa majeruhi ya msuli.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini bahati haikuwa yetu mara baada ya kushuhudia tukifungwa goli la pili mara baada ya mpira kumdunda Rudiger na kumkuta Xhaka aliyefunga kilaini kabisa..
Kwa matokeo hayo yanaifanya Arsenyani kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Chelsea katika kombe la ligi toka mwaka 1998.
No comments:
Post a Comment