Kocha wa Chelsea, Antonio Conte jioni ya leo atakuwa kwenye benchi kuiongoza timu yake kumenyana dhidi ya klabu ya Leicester city katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa raundi ya 23 ambao utachezwa saa 12 jioni ya leo.
Kocha huyo kuelekea katika mchezo huo ameulizwa juu ya hatima ya nyota wa klabu hiyo, Michy Batshuayi anayeonekana kuwa na ugumu kupata nafasi katika kikosi cha klabu hiyo ambapo mpaka sasa amecheza michezo 11 huku akianza michezo miwili tu na kufanikiwa kufunga magoli 2 katika ligi kuu Uingereza.
"Kwenye maisha lazima kuwe na ushindani, haswa kwenye klabu kubwa kama Chelsea, lazima ushindani uwepo haswa kuwa mchezaji wa hapa maana kwa nafasi yako lazima kuwe na mchezaji zaidi ya mmoja. Kwa nafasi ya Batshuayi kuna washambuliaji wawili na nusu, hiyo nusu ni kwa maana ya Eden Hazard ambaye yeye anaweza kucheza katika nafasi hiyo inapobidi.
"Kwa Morata ni mchezaji mdogo na kucheza msimu mzima kama mshambuliaji wa kati akitegemewa katika nafasi hiyo ni mara chache kwake na hii ndio mara ya kwanza. Kwa upande wa Michy naye ni hivyohivyo, alicheza msimu mzima mara moja tu akiwa klabuni Marseille, tunajua yupo kwenye hali gani ila la muhimu kwa sasa ni kupambana zaidi ili awape presha wenzake" alisema kocha Antonio Conte.
Michy Batshuayi alisajiliwa akitokea klabu ya nchini Ufaransa inayoshghiriki ligi kuu nchini humo kwa dau la paundi milioni 35 na mpaka sasa yupo Chelsea akiwa na msimu wa pili huku akiisaidia kutwaa taji la ligi kuu Uingereza akifunga goli la muhimu katika mchezo dhidi ya West Bromwich msimu uliopita.
CONTE AONGELEA NAFASI YA BATSHUAYI NDANI YA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment