HABARI MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs LEICESTER - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA CHELSEA vs LEICESTER

Share This
Kuelekea mchezo wa leo jioni pale Stamford Bridge kati ya Chelsea ikiikaribisha klabu inayomilikiwa na tajiri wa kiasia, Leicester city wanaotokea pale King Power, hapa nakuletea habari muhimu za kuzifahamu kuelekea katika mchezo huo ambao Chelsea itahitaji ipate ushindi ili ijiweke sehemu nzuri katika msimamo wa ligi kuu ambapo kama itashinda na mchezo huu basi itapanda mpaka nafasi ya pili na kufikisha alama 49.

Habari muhimu;
Chelsea; Chelsea itashuka katika mchezo huu ikiwa kamili bila kuwa na mchezaji yoyote aliye majeruhi, hata Ross Barkley ambaye alisajiliwa akiwa na majeruhi nae anaonekana kuwa sawa mara baada ya kuanza mazoezi na klabu ila jana kocha Antonio Conte alisema nyota huyo anaweza akacheza mchezo wake wa kwanza toka msimu huu uanze dhidi ya Norwich katika raundi ya nne ya kombe la FA. Gary Cahill anaweza akaanza katika mchezo huu mara baada ya kupumzishwa katikamchezo wa jumatano ambapo Chelsea ilishuka uwanjai kumenyana na Arsenyani(Arsenal) katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la ligi, Carabao.
Leicester; Vijana hawa wa King Power watashuka katika mchezo huu huku wakiwa na mfululizo wa matokeo mabovu na majeruhi kibao. Wes Morgan, Robert Huth, Christian Fuchs, Vicente Iborra, na Danny Simpson huku Jamie Vardy akiwa kucheza mchezo wa leo.

Mwamuzi; Mike Jones ndiye atakuwa mwamuzi wa kati katika mchezo huu wa leo huku akiwa na miaka 49 mpaka sasa, lakini jambo la kushangaza kuhusu yeye alianza kuwa mwamuzi akiwa na miaka 9 tu, hiyo ilikuwa mwaka 1997. Lakini kwa upande wa Chelsea huu ndio utakuwa mchezo wake wa kwanza kwa msimu huu ambapo msimu uliopita alikuwa mwamuzi katikamchezo wa siku ya 'Boxing Day' huku katika mchezo huo Chelsea iliitadika Bournemouth mabao 3-0 huku pia akihusika katika michezo 17 msimu huu ambao katika michezo hiyo ametoa kadi 62 za njano na kadi nyekundu moja.

Mchezo uliopita; Katika mchezo uliopita Chelsea iliibamiza Leicester city mabao 2-1 huku Leicester akiwa nyumbani kwake. Magoli ya Chelsea yalifungwa na Alvaro Morata na N'Golo Kante.

H2h; Tangu dunia imeingia mwaka 2000 mpaka leo tupo mwaka 2018, Chelsea imepoteza michezo mitatu tu ndani ya miaka 18 huku ikishinda michezo 12 na kutoa suluhu michezo miwili dhidi ya Leicester huku mara ya mwisho kwa Leicester kupata ushindi dhidi ya Chelsea ilikuwa mwaka 2015.

Rekodi;
Chelsea: WWDDD

Leicester:  DLLWD

Muda; Saa 06:00 Jioni(Saa 18:00)





No comments:

Post a Comment