Kumekuwa na vita ya maneno inayoendelea kati ya kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Manyumbu(Man utd) dhidi ya kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte ambapo vita yao ya maneno imekuwa kivutio wakati kwa wengine wanaona haina maana yoyote. Lakini nyota wa Chelsea, Eden Hazard alipoulizwa juu ya vita hiyo ya maneno inayoendelea kati ya makocha hao ambao amewai kufundisha nao wote huku mmoja akiwa bado ni kocha wake klabuni Chelsea.
"Kuna makocha wengi wanaingia katika vita ya maneno kama wanavyofanya wao, hilo kwangu halinihusu, kikubwa nachoangalia mimi kama mchezaji natakiwa kucheza uwanjani na kuhakikisha timu inapata matokeo yanayostahili" alijibu Hazard alipoulizwa juu ya ugomvi huo.
Conte na Mourinho wamekuwa na mfululizo wa maneno huku kila mtu akikejeli juu ya uwezo wa mwengine, je kwa upande wako unaona kuna usahihi katika vita hii?
HAZARD AWAPA VISOGO CONTE NA MOURINHO
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment