Chelsea iliyokuwa chini ya kocha muitaliano, Claudio Ranieri ilifanikiwa kumnasa nyota wa kifaransa William Gallas kutoka klabu ya Olympique Marseille ya nchini kwao Ufaransa ambapo dau la paundi milioni 6 likatumika kumvuta nyota huyo klabuni Chelsea ambapo alitengeneza ukuta imara akiwa na mfaransa mwenzake Marcel Desailly kabla ya baadae kusimama sambamba na John Terry. Mwaka 2001 alitua Chelsea.
Mwaka 2006 aliondoka Chelsea kwa mgogoro mkubwa ambapo alikataa kuongeza mkataba huku klabu kadhaa kutoka ligi kuu ya Italia kuonyesha nia ya kumtaka lakini Chelsea iligoma na kumpeleka Arsenal ambapo kupelekwa kwake huko alitumika kama mabadilishano ili Chelsea imnase Ashley Cole. Kwa akili ya kawaida unaweza ukafikiri Chelsea ndio klabu atakayokua anaichukia maana kuondoka kwake hapo kulizuka maneno ambapo inadaiwa Chelsea walimsikia mchezaji huyo akisema kama asipouzwa basi atajifunga goli kwa makusudi.
La Hasha! Moja kati ya mahojiano aliyofanyiwa baada ya kustaafu soka aliishia kusema hakuna timu ya Uingereza ya jijini London anayoipenda kama Chelsea licha ya kuzichezea Arsenal na Tottenham ambazo zote zinapatikana London.
Sasa tena ili kuonyesha mapenzi yake kwa Chelsea, mfaransa huyo amethibitisha kuwa mmoja wa wachezaji kwenye kikosi cha wakongwe wa Chelsea wanaojiita Chelsea Legends kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wakongwe wa Inter Milan wanaojiita Inter Forever.
Gallas ataungana na nyota wengine kama Gianfranco Zola, Michael Ballack, Dennis Wise, Eidur Gudjonsen pamoja na wengine wengi siku ya tarehe 18-May mwaka huu, mchezo utachezwa pale Stamford Bridge.
**********
Zimesalia siku 3 ili kushiriki kampeni yetu ya kuchangia damu kwa hiyari ambapo kampeni hiyo iliyochini ya blog hii ya Darajani 1905 inayoitwa "Charity For The Blues" itakayofanyika tarehe 19-May pale kwenye hospitali ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment