Chelsea imeshindwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao mara baada ya kumaliza kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo Chelsea iliyochini ya kocha Antonio Conte ikishindwa kulitetea taji hilo ililoshinda msimu uliopita.
Lakini je unajua sababu iliyoifanya Chelsea kushindwa kufudhu kucheza michuano hiyo ya barani Ulaya kwa msimu ujao? bila shaka kuna sababu nyingi lakini kocha Antonio Conte ameitaja moja ya sababu iliyosababisha Chelsea kuwa na msimu mbaya.
Akifanyiwa mahojiano kabla ya mchezo wa mwisho wa ligi kuu ambapo Chelsea ilipoteza kwa magoli 3-0 dhidi ya Newcastle iliyokua nyumbani, kocha Conte alisema "Kumpoteza Michael lilikua ni jambo baya kwetu"
"Michael (Emenalo) amefanya kazi kubwa sana katika hii klabu, amekua hapa kwa muda mrefu na hata msimu ujao alikuwa msaada mkubwa sana kwangu, pia msimu huu amekua akinisaidia sana mpaka pale alipoondoka mwezi Oktoba. Ilikuwa ni pigo kubwa sana kwetu. Nakumbuka sana wakati alipoondoka ilikuwa ni baada ya ushindi dhidi ya Manchester united" alisema kocha huyo muitaliano.
Lakini pia mlinzi wa Chelsea ambaye ni raia wa Denmark, Andreas Christensen aliwai kuelezea mchango mkubwa na kwanini anaona Michael Emenalo hakustahili kuondoka Chelsea ambapo hii ni sawa na maneno anayoyazungumza kocha Antonio Conte.
Lakini pia hii inaonyesha kwa kiasi gani kikubwa mashabiki wengi wa Chelsea walikosea pindi walipokua wanampiga vita Michael Emenalo ambaye kazi yake klabuni Chelsea kama mkurugenzi wa benchi la ufundi aliisaidia Chelsea kushinda mataji kama ligi kuu Uingereza mara tatu, klabu bingwa barani Ulaya (UEFA Champions League), ligi ya Ulaya (Europa League), kombe la FA pamoja na kombe la ligi.
Na mwafrika huyo baada ya kuandika barua ya kujiuzulu klabuni Chelsea mwezi Oktoba-2017 alitangazwa kujiunga na klabu ya As Monaco huku nafasi yake klabuni Chelsea ikichukuliwa na mwanamama Marina Glanovskaia.
No comments:
Post a Comment