Kumekuwa na wasiwasi mkubwa juu ya nyota wa Chelsea, Eden Hazard kama ataendelea kusalia klabuni Chelsea mara baada ya klabu hiyo kushindwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.
Hatimaye nyota huyo amevunja ukimya na kueleza kama ataendelea kusalia klabuni hapo kwa msimu ujao au atatazamia kuondoka klabuni hapo.
"Na ndio maana nachukua muda zaidi katika hili (juu ya kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea), ni jambo kubwa sana kwa hiyo ninahitaji muda wa kufikiria mambo mengi. Lakini jambo moja nna uhakika nalo, kwamba nna furaha kubwa ya kuwa klabuni hapa"
"Nasubiri wachezaji wapya kwa msimu ujao. Unajua, tutaona. Nahitaji kucheza na wachezaji wazuri kwa sababu nahitaji nishinde ligi kuu Uingereza." alisema winga huyo raia wa Ubelgiji.
Hata hivyo nyota huyo aliulizwa pia kama kusalia au kuondoka kwa kocha Antonio Conte klabuni Chelsea kama kutamfanya winga huyo asaini mkataba mpya, nyota huyo alijibu akisema "Sifikirii katika hilo. Kwa sasa tunawaza na kufikiria kuhusu mchezo ujao. Tumebakiza mchezo mmoja na tutaona kipi kitatokea ifikapo mwishoni mwa msimu na mwanzoni mwa msimu" alisema Hazard.
Klabu ya Chelsea imekua ikieleza kuwa ipo tayari kumpa mkataba mpya nyota huyo huku ikimpa ofa ya mshahara wa paundi 300,000, mshahara utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi klabuni Chelsea huku mkataba wake wa sasa ukiwa unaisha mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment