Klabu nyingi nchini Uingereza zimeshamaliza msimu wa 2017-2018 ambapo hazina michezo ya kimashindano zaidi ya kucheza michezo ya kirafiki ili kujiandaa na msimu mpya wa 2018-2019, lakini kuna klabu tatu bado hazijakamilisha msimu ambazo ni pamoja na Liverpool ambao wamebakiza kucheza fainali ya klabu bingwa na nyengine ni pamoja na Chelsea pamoja na Manchester united ambazo zitamenyana uso kwa uso kwenye fainali ya kombe la FA itakayochezwa jumamosi hii ya tarehe 19-May.
Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio nafasi pekee ya Chelsea kuweza kushinda taji lake pekee msimu huu, kiungo wake, Cesc Fabregas amewahamasisha wenzake na kutoa ujumbe mzito kwa klabu nzima ya Chelsea juu ya fainali hiyo.
"Kuna moto (hali ya kupambana) inayotakiwa kila mtu awe nayo, kila mtu inatakiwa ajisikie njaa ya mafanikio ndani yake, na hali hiyo siwezi kuifanya mimi au kocha kwamba watu wajisikie hivyo"
"Inawezekana moto huo ukawa nao au usiwe nao lakini jumamosi kila mchezaji inatakiwa aonyeshe mapambano na kupambana katika mchezo huo. Nina uhakika kwa 100% siku hiyo sio maalumu kuwaambia wachezaji wacheze mchezo mzuri maana hilo ni jukumu letu na tunaupenda mchezo huu kwa 120%. Ni fainali, utakuwa ni mchezo mgumu lakini muhimu kucheza kwa kupambana" alisema mhispania huyo.
Chelsea itashuka kwenye mchezo huo huku ikiendelea kuwakosa nyota wake David Luiz anayesumbuliwa na majeraha ya mguu lakini pia Ethan Ampadu akiendelea kukosekana.
No comments:
Post a Comment