Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies wamefanikiwa kutwaa taji la ligi kuu kwa wanawake (FA WSL) kwa msimu wa 2017-2018 usiku wa leo mara baada ya kupata ushindi wa mabao 0-2 ikiwa ugenini dhidi ya Bristol city.
Klabu hiyo ya soka imejipatia goli lake la kwanza kupitia kwa nyota wake Spence aliyefunga vyema kwa goli la kichwa na kuifanya Chelsea iondoke mapumziko ikiwa inaongoza kwa goli 0-1. Goli la pili la Chelsea lilifungwa na Joanna Anderson ambae aliihakikishia kikosi chake ubingwa huo wa ligi kuu huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote.
Hili ni taji la pili kwa Chelsea Ladies ambapo mpaka sasa ikiwa imebakiza mchezo mmoja wa ligi kuu imeshajihakikishia rasmi kuwa mabingwa wa ligi hiyo huku siku kadhaa ikitoka kuibamiza Arsenal Ladies kwa mabao 3-1 na kushinda taji la kombe la FA kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
No comments:
Post a Comment