Inasadikika kuwa tajiri na mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich anataka kuiuza klabu hiyo ambapo sababu kubwa inayotajwa ni kutokana na kibali chake cha kuishi nchini Uingereza kuisha huku pia ikidaiwa ameamua kuanza makazi mapya nchini Israel ambapo huko amejenga jumba la kifahari.
Hatimaye kukaripotiwa tajiri mmoja ambaye ni mtoto wa mtu mashuhuri nchini Dubai alitaka kuinunua klabu hiyo, sasa ameibuka tajiri mwengine kutoka nchini Uingereza ambaye huyo ni tajiri zaidi nchini Uingereza, Jim Ratcliffe ambaye ametangaza kuinunua klabu hiyo. Lakini imeripotiwa kuwa Abramovich amekataa kuiuza klabu hiyo.
Jim Ratcliffe ambaye ana utajiri unaofikia paundi bilioni 20 wakati Abramovich ana utajiri wa paundi bilioni 9 anataka kuinunua Chelsea huku akiwa shabiki wa Manchester united ingawa amekuwa akiifatilia sana Chelsea na ndiyo maana amekuwa akikata tiketi za mwaka mzima za Chelsea na amekuwa akitembelea uwanja wa mazoezi wa Chelsea maarufu kama Cobham.
Sababu mojawapo inayotajwa kumfanya kuvutiwa na Chelsea ni ukaribu wa klabu hiyo ilipo na makazi yake yalipo. Anamiliki kampuni ambayo huingiza faida zaidi ya paundi bilioni 45 huku akiwa na wafanyakazi 18,500 kwenye mataifa 22.
No comments:
Post a Comment