Kikosi cha vijana wa timu ya taifa ya Uingereza wenye umri chini ya miaka 21 wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 vijana wa Mexico na kufanikiwa kutwaa taji la kombe la Toulon.
Uingereza wamefanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo huku safari hii ikiwajumuisha nyota watatu kutoka Chelsea ambao ni Tammy Abraham ambaye msimu uliopita aliitumikia kwa mkopo klabu ya Swansea, Billy Gilmour ambaye bado yupo kwenye akademi ya Chelsea na yeye ndiyo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo pamoja na Jake Clarke-Salter ambaye msimu uliomalizika ameitumikia klabu ya Sunderland kwenye ligi daraja la kwanza pale Uingereza maarufu kama Championship.
Hongereni vijana...
No comments:
Post a Comment