Nyota wa kikosi cha Chelsea FC Women, Erin Cuthbert ameiongoza vyema timu yake ya taifa ya Scotland kupata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Belarus katika mchezo wa kugombania kufudhu kucheza kombe la dunia kwa wanawake litakalofanyika mwaka 2019.
Cuthbert aliisaidia timu hiyo kuondoka na ushindi huo huku mwenyewe akiwa mfungaji wa magoli hayo mawili yanayoifanya Scotland kusogea mpaka kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa makundi ya kugombania kufudhu.
Belarus ambao wanashika mkia kwenye kundi hilo ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza katika dakika ya 27 kabla ya Cuthbert kusawazisha na kufanya mchezo kwenda mapumziko kwa sare ya 1-1.
Katika kipindi cha pili, Cuthbert alihitaji dakika 20 tu za kipindi cha pili ili kuifanya timu yake kupunguza pengo hilo la alama ambapo kwa sasa Scotland inaachwa kwa alama tatu tu dhidi ya New Zealand.
No comments:
Post a Comment