CONTE HAONDOKI CHELSEA - Darajani 1905

CONTE HAONDOKI CHELSEA

Share This
Licha ya habari nyingi kuzagaa zikimhusisha kocha wa Chelsea, Antonio Conte kuondoka klabuni hapo, kumetoka taarifa mpya zinazoripoti kuwa hakuna kinachoendelea juu ya mipango ya kutimuliwa kocha huyo na anategemewa kuendelea kuwa kocha wa Chelsea.
Taarifa hizo zilizogaa kwenye vyombo vya habari duniani, vinaripoti kuwa Chelsea haina mpango wa kumtimua kocha huyo licha ya matokeo mabovu toka kuingia kwa mwaka 2018, mpaka sasa Chelsea imefululiza kucheza michezo 10 huku ikipata ushindi mara mbili, lakini yote hayo bado Chelsea ipo kwenye klabu nne za msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo kwa nafasi hiyo itamfanya ashiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya msimu ujao, lakini pia kwa msimu huu ipo katika hatua ya 16-bora ambapo itamenyana dhidi ya Barcelona katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Nahodha wa Chelsea, Gary Cahill amemtetea kocha huyo juu ya kiwango kibovu kinachoonyeshwa na Chelsea kwa sasa ambapo amekaririwa akisema wanaopaswa kulaumiwa ni wachezaji maana kocha anafanya kazi yake vyema. Lakini pia mlinda mlango namba moja wa Chelsea, Thibaut Courtois nae anamtetea kocha Antonio Conte.

No comments:

Post a Comment