Kinda wa Chelsea aliyeko Swansea City kwa mkopo,Tammy Abraham ameshindwa kufunga bao lolote katika timu hiyo ya Swansea tangu katikati ya mwezi wa kumi mwaka jana na kuweza kupoteza namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Abraham (20) alianza vyema kampeni ya ufungaji wa mabao tangu ajiunge na timu hio ambapo alifunga mabao 5 katika miezi miwili ya kwanza tangu atue klabuni na pia kupata nafasi timu ya taifa ya England na kucheza michezo miwili dhidi ya Ujerumani na Brazili mnamo mwezi november ya mwaka uliopita.
Kocha mkuu wa timu hiyo Carlos Carvalhal amemjia juu mchezaji huyo na kutaka afanye bidii na kuacha kubweteka kama anataka kuwa mchezaji mkubwa kama Christiano Ronaldo.
" Nimeongea na Abraham na anajua nini afanye ili aweze kuwa katika kikosi cha kwanza na mchezaji aliyekamilika. Kama atafanya vile tunavyomuelekeza basi atakuwa moja ya mchezaji mkubwa mbeleni", Alinukuliwa Kocha huyo.
Pia kocha huyo alisisitiza kwamba Abraham ataanza katika mchezo wa FA raundi ya nne dhidi ya Notts County hapo jummane.
No comments:
Post a Comment