Kumekuwa na taarifa nyingi zikimhusu kocha wa Chelsea, Antonio Conte kuondoka klabuni Chelsea muda mfupi kuanzia sasa huku nafasi yake ikitajwa kuchukuliwa na kocha wa zamani wa klabu ya Barcelona inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania, tetesi hizo zinakuja muda fupi mara baada ya kocha huyo kushuhudia Chelsea ikipoteza mchezo wake wa pili katika ligi kuu Uingereza (dhidi ya Bournemouth na Watford).
Kutokana na mfululizo huo wa matokeo mabaya, inaonekana nafasi ya kocha Antonio Conte kuendelea kubaki Chelsea ni finyu huku ikiripotiwa kocha huyo ana mgogoro pia na bodi ya klabu hiyo huku chanzo kikubwa kikitajwa jinsi mfumo wa usajili ulivyo klabuni hapo ambapo usajili wote unakamilishwa na bodi, na kazi ya kocha Conte ni kupendekeza tu mchezaji wa aina gani anamtaka.
Mara baada ya vuguvugu hilo, nahodha wa Chelsea ambaye ni raia wa Uingereza, Gary Cahill amemtetea kocha Antonio Conte juu ya matokeo mabovu klabuni hapo.
"Najisikia vibaya sana. Kuwa hapa alafu ukashuhudia klabu inacheza katika kiwango kibovu, inaumiza na inasikitisha ila sisi wachezaji ndio tunatakiwa kulaumiwa. Kocha amekuwa akifanya kazi kwa hali ya juu" alisema nahodha huyo mwenye miaka 31.

CAHILL AMUONGELEA CONTE JUU YA KIWANGO KIBOVU CHA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment