Mara baada ya Chelsea kupata matokeo mabovu usiku wa jana ikipoteza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza ikiwa ugenini dhidi ya Watford, kocha Antonio Conte amewapa ofa wachezaji wa klabu hiyo akiwapa siku tatu za mapumziko ili kuwafanya wapumzike kutokana na kuwa ratiba iliyofululiza michezo mingi kwa muda mfupi.
Kocha Antonio Conte amekutana na wachezaji wa Chelsea leo katika uwanja wa Cobham na kuwapa ofa hiyo ili kuwapa muda wa kupumzika zaidi ili kuwa sawa akiamini kufululiza kwao kucheza michezo mingi kunawafanya wachezaji kucheza chini ya kiwango.
Katika mchezo wa jana alimpumzisha Marcos Alonso ambaye hakucheza mchezo huo kutokana na kocha huyo kuamini kuwa amecheza michezo mingi kwa maana hiyo akaamua kumpumzisha, lakini mfumo huo wa kuwapumzishawachezaji amekuwa nao kwa muda sasa akitumia wachezaji tofautitofauti katika kikosi cha kuanza.

CONTE APATA DAWA YA WACHEZAJI WA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment