MRITHI WA CONTE KUICHUKUA TIMU MUDA WOWOTE KUANZIA SASA - Darajani 1905

MRITHI WA CONTE KUICHUKUA TIMU MUDA WOWOTE KUANZIA SASA

Share This
Kuna taarifa zinadai kuwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte anaweza akatimuliwa klabuni hapo katika masaamachache yajayo mara baada ya mfululizo wa matokeo mabovu ambapo usiku uliopita ametoka kuiongoza Chelsea kupoteza mchezo wake dhidi ya Watford kwa magoli 4-1 huku mchezo mwengine wa ligi kuu Uingereza uliopita alishuhudia kipigo cha magoli 3-0 dhidi ya afc Bournemouth.

Gazeti moja la nchini Hispania linamtaja kocha wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique kuchukua nafasi ya kocha huyo klabuni Chelsea ambapo Eneique kwa sasa amekuwa mapumzikoni kutokana na kuachana na Barcelona mwishoni mwa msimu uliopita.

Mazimiliano Sarri ambaye ni kocha wa Napoli anatajwa kuwaniwa na Chelsea kabla ya mmiliki wa klabu ya Napoli kudai atafanya mazungumzo na kocha huyo ili kumbakisha ingawa taarifa zinadai kuwa Roman Abramovich ambaye ni mmiliki wa Chelsea anamtazama Sarri kama chaguo lake pia.

Makocha wengine wanaotajwa kuwaniwa na Chelsea ni pamoja na Carlo Ancellotti ambaye amekataa kujiunga na timu za taifa, Massimiliano Allegri ambaye aliwai kuhojiwa juu ya kujiunga na Chelsea ingawa mwenyewe alikataa na kusema bado ana furaha ya kubaki kwenye klabu ya Juventus ambayo ndiyo anaifundisha kwa sasa.

No comments:

Post a Comment